IQNA

Mafunzo ya kuhifadhi Qur’ani UAE kufanyika kwa njia ya intaneti

21:00 - March 17, 2020
Habari ID: 3472575
TEHRAN (IQNA) – Mafunzo ya kuhifadhi Qur’ani Tukufu katika Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) yatafanyika kwa njia ya intaneti baada ya misikiti na vituo vya Kiislamu kufungwa nchini humo kutokana na hofu ya kuenea ugonjwa wa COVID-19 au corona.

Kwa mujibu wa taarifa ya Kituo cha Qur’ani cha Hamid bin Rashed al-Naeemi, mafunzo ya kuhifadhi Qur’ani  yatafanyika kwa njia ya intaneti katika kipindi cha miezi michache ijayo.

Taarifa hiyo imesema kituo hicho kitatoa mafunzo ya kuhifadhi Qur’ani kupitia intaneti  kwa wavulana na wasichana 120. Mkurugenzi wa kituo hicho, Ezza bint Abdullah al-Naeemi amesema hatua hiyo inalenga kuwawezesha vijana kuendelea kuhifadhi Qur’ani na kupata taaluma zingine za Qur’ani pamoja na kuwepo vizingiti nchini humo kufuatia kuenea kirusi cha corona.

Siku ya Jumatatu UAE ilitangaza marufuku ya sala za jamaa katika misikiti ya nchi hiyo kwa muda wa mwezi moja ili kuzuia kuenea kirusi cha corona. Hadi sasa watu 98 wameambukizwa corona katika nchi hiyo ya Ghuba ya Uajemi.

3470934

captcha