IQNA

Kiongozi Muadhamu awashukuru maafisa wote wa afya Iran kutokana na jitihada za kukabiliana na corona

19:44 - March 29, 2020
Habari ID: 3472612
TEHRAN (IQNA) - Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kuwa, mpango wa kuwachunguza watu kiafya nchini Iran kwa ajili ya kukabiliana na ugonjwa wa COVID-19 au kirusi cha corona ni kazi kubwa ya kujivunia.

Ayatullah Sayyid Ali Khamenei leo amwandikia barua Waziri wa Afya wa Iran, Daktar Said Namaki na huku akiwashukuru maafisa wote wa afya na matibabu humu nchini amesema, kutumiwa uwezo wa vikosi vy Basiji na vya kujitolea vya wananchi kutazidi kulisaidia taifa na kuliweka salama katika wimbi hili la maambukizi ya kirusi cha corona.

Ayatullah Khamenei vile vile amesisitiza kuwa, kuna haja ya kuendelea jitihada zinazofanyika katika kila kona humu nchini katika kupambana na kirusi cha corona na amemuomba Mwenyezi Mungu awalinde wafanyakazi wa afya humu nchini na kuwapa ushindi, afya njema na usalama katika kazi hii kubwa wanayoendelea kuifanya.

Wakati huo huo Daktari Kianoush Jahanpour, Msemaji wa Wizara ya Afya ya Iran  amesema kuwa, hadi hivi sasa zaidi ya watu milioni 50 wameshafanyiwa uchunguzi wa kiafya na kupimwa corona nchini Iran katika juhudi za nchi nzima za kupambana na ugonjwa wa COVID-19.

Mbali na hatua nyingi za kinga, serikali ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa kusaidiana na vikosi vya ulinzi humu nchini imechukua hatua nyingine nyingi muhimu kama vile kupunguza sana muda wa kutoa majibu ya vipimo vya corona, kutenganishwa wagonjwa, kutoa matibabu ya haraka na jitihada nyingine nyingi ambapo licha ya mashinikizo makubwa waliyowekewa wananchi wa Iran na hasa na dola la kibeberu la Marekani, lakini juhudi za kupambana na corona zinaendelea vizuri nchini Iran.

3888082

captcha