IQNA

Waislamu watakiwa walinde mafanikio yaliyopatikana Mwezi wa Ramadhani

16:19 - May 26, 2020
Habari ID: 3472804
TEHRAN (IQNA) – Mwakilishi wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini India amesisitiza umuhimu wa Waislamu kudumisha mafanikio waliyoweza kuyapata katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Katika ujumbe kwa mnasaba wa Siku Kuu ya Idul Fitr, Hujjatul Islam Mahdi Mahdavipour amessema Mwezi Mtukufu wa Ramadhani ni mwezi wenye baraka tele  na ni wakati ambao Waislamu hujibiddisha katika ibada na kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu SWT.

Amesema moja ya mafanikio makubwa ya Ramadhani kwa muumini ni kuwa karibu zaidi ya dhati au fitra yake ambayo ni  kumcha Mwenyezi Mungu na hivyo kunapaswa kuwepo jitihada za kudumisha hali hiyo.

Hujjatul Islam Mahdavipour amewapongeza Waislamu wote kwa mnasaba wa siku kuu ya Idul Fitr na kuongeza kuwa kwa baraka za duaa za waumini, janga la COVID-19 litamalizika kote duniani.

3901240/

Kishikizo: ramadhani india waislamu
captcha