IQNA

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu

Mafanikio ya Demokrasia ya Kiislamu yameivutia dunia nzima

15:42 - May 27, 2020
Habari ID: 3472807
TEHRAN (IQNA) – Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Sayyed Ali Khamenei ametuma salamu za pongezi katika sherehe za kuanza awamu ya 11 ya Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu, Bunge la Iran, na kusema kwa mara nyingine, demokrasia ya Kiislamu imeonyesha mvuto wake duniani.

Katika ujumbe wake uliosomwa bungeni leo Jumatano mjini Tehran Ayatullah Sayyid Ali Khamenei amesema, 'duru ya 11 ya Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu imeanza na kwa mara nyingine mvuto na nuru ya demokrasia ya Kiislamu imeonyesha mvuti wake kwa dunia nzima. Namshurkuru Allah SWT kwa kulisaidia taifa la Iran katika jitihada zake za kuunda Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu."

Katika ujumbe huo  uliosomwa na Mkuu wa Ofisi ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Hujjatulislam Mohammadi Golpayegani, Kiongozi Muadhamu amewahutubu Wabunge hao akiwaambia: Mnapaswa kuandaa mikakati ya kuboresha maisha ya watu wenye mahitaji, na hili kwa mujibu wa wataalamu wa masuala ya uchumi, linawezekana tu kwa kuangalia upya njia mpya za kuunua uchumi wa taifa kama kubuniwa nafasi za ajira, uzalishaji, thamani ya sarafu ya taifa, na kudhibiti mfumko wa bei za bidhaa.

Kadhalika amelitaka Bunge hilo liwe na ushirikiano wa karibu na mihimili mingine ya serikali, yaani Baraza la Mawaziri na Vyombo vya Mahakama.

Aidha Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameliasa Bunge hilo lisishughulishwe zaidi na mambo madogo yasio na maslahi kwa wananchi wa kawaida, sanjari na kutorohusu masuala ya kibinafsi, kichama na kimrengo kuteka ajenda za mijadala ya taasisi hiyo muhimu ya kutunga sheria.

Ayatullah Sayyid Ali Khamenei katika ujumbe wake amesisitiza kuwa 'uchumi na utamaduni' ni mambo ambayo yanapaswa kupewa kipaumbele nchini na kuongeza kuwa: Wabunge wanapaswa kutoa kipaumbele kwa masuala ya kimaisha ya tabaka la watu dhaifu, kufanya marekebisho katika nukta muhimu za uchumi kama vile ajira, uzalishaji na mfumuko wa bei, kuzingatia taqua na insafu katika wa kutekeleza majukumu ya usimamizi, misimamo ya kimapinduzi katika matukio muhimu na kuwa na ushirikiano wa kidugu na mihimili mingine ya dola ambayo ni serikali na vyombo vya mahakama.

Kiongozi Muadhamu ameashiria jukumu jingina la bunge au Majlisi ambalo ni kutayarisha 'Mpango wa Tano wa Ustawi wa Nchi' na kuwahutubu wabunge kwa kusema: Nasaha yangu kwenu ni hii kuwa, mzingatie kupungua nafasi ya mafuta ghafi ya petroli katika pato la serikali kuwa ni fursa kwa ajili ya kurekebisha uchumi wa nchi."

3471531

captcha