IQNA

12:10 - May 29, 2020
News ID: 3472812
TEHRAN (IQNA) - Aya za Qur'ani Tukufu zimesomwa katika Kanisa Kubwa la Hagia Sophia ambalo sasa ni jumba la makumbusho mjini Istanbul Uturuki.

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdoogan amesema aya hizo zitasomwa kwa mnasaba wa kutekwa mji huo mwaka 1453.
Erdogan amesema mara kadhaa kuwa jengo la Hagia Sophia ambalo ni Turathi ya Dunia ya UNESCO, na sasa ni jengo la makumbusho linaweza kubadilishwa tena na kuwa msikiti.
Hagia Sophia ni jina la Kigiriki la kanisa kubwa mjini Istanbul - Konstantinopoli lililobadilishwa kuwa msikiti tangu 1453 na halafu kuwa makumbusho mwaka 1934.
Mwaka 1453 Waturuki Waislamu waliteka mji wa Konstantinopoli na kuifanya mji mkuu wa Dola la Osmani. Hapo Hagia Sofia likabadilishwa kuwa msikiti na Waturuki wakatamka jina la kigiriki kama "Ayasofya". Jengo la kanisa likaongezekwa minara minne ya mtindo wa Kiislamu.
Baada ya anguko la Waosmani katika vita kuu ya kwanza ya dunia kiongozi wa taifa Kemal Atatürk akaamuru jengo liwe makumbusho mwaka 1935. Kila mwaka mamilioni ya watalii hutembelea jengo hilo.

3471538

Name:
Email:
* Comment:
* captcha: