IQNA

Watunisia waibuka kutoka zuio la COVID-19, wamiminika misikitini, migahawani

21:15 - June 04, 2020
Habari ID: 3472835
TEHRAN (IQNA) – Wananchi wa Tunisia wamerejea katika misikiti na migahawa Alhamisi baada ya nchi hiyo kuhitimisha zuio na vizingiti ambavyo vilikuwa vimewekwa kuzuia kuenea ugonjwa wa COVID-19.

Mwezi Machi Tunisia ilifunga mipaka yake yote ya kimataifa, ikasitisha safari baina ya miji, ikaamuru kufungwa misikiti, shule, maduka na migahawa na sheria ya kutotoka nje ikaanza kutekelezwa usiku.

Nchi hiyo ina kesi 1,048 za COVID-19 na vifo 48 hiyo ikiwa ni idadi ndogo ya maambukizi ikilinganishwa na chi jirani ya Algeria yenye kesi 10,000 na vifo zaidi ya 670.

Pamoja na kuwa misikiti na migahawa imefunguliwa, serikali ya Tunisia imesema shule zitaendelea kufungwa hadi kuanza mwaka mpya wa masomo mwezi Septemba na pia ni marufuku kuwa na mijumuiko mikubwa majumbani huku wananchi wakihimizwa kuendelea kuvaa barakoa na kutii sheria za kiafya za kuzuia maambukizi ya corona. Mipaka yakimataifa ya Tunisia inatazamiwa kufunguliwa mwishoni mwa mwezi huu wa Juni.

/3471596

captcha