IQNA

Misikiti ya New Jersey Marekani kuhubiri kuhusu ubaya wa ubaguzi na ukatili unaotendwa na polisi

14:44 - June 05, 2020
Habari ID: 3472837
TEHRAN (IQNA)- Misikiti kadhaa kote katika jimbo la New Jersey nchini Marekani imesema hotuba za Sala ya Ijumaa zitajadili kuhusu madhara ya ubaguzi wa rangi na halikadhalika kuhusu ukatili na jinao zinazotendwa na polisi nchini humo.

Kwa mujibu wa taarifa ya mashirika kadhaa ya Kiislamu hotuba za leo ambayo imetakwa kuwa  ni ‘Ijumaa ya Ghadhabu’ ni sehemu ya mpango wa Waislamu kubainisha mshikamano wao na Wamarekani wenye asili ya Afrika baada ya mauaji ya kinyama ya George Floyd.

Wiki iliyopita, afisa mmoja mzungu wa jeshi la polisi la Marekani, anayejulikana kwa jina la Derek Chauvin, alimuua kikatili na kwa damu baridi kabisa, George Floyd Mmarekani mwenye asili ya Afrika katika mji wa Minneapolis huku wenzake watatu wakitizama na kuwazuia wapita njia wasimuokoe Mmarekani huyo. Ukatili huo umezusha wimbi kubwa la maandamano na machafuko katika kona zote za Marekani na sasa Rais Donald Trump ametangaza serikali ya kijeshi.

Selaedin Maksut, mkurugenzi wa tawi la New Jersey la Baraza la Mahusiano ya Kiislamu Marekani (CAIR) amesema: “Tunataka kuwahimiza viongozi Waislamu kutoa taarifa za kulaani ukatili wa polisi na ubaguzi wa rangi. Aidha tunawataka wapambana na ubaguzi katika jamii za Waislamu.”

Karibu taasisi 60, zikiweemo zinazowakilishia misikiti, zilitia saini waraka wa Juni 3 wa kuafiki kuunga mkono jitiahda za kuunga mkono Wamarekani weusi au wenye asili ya Afrika sambamba na kukabiliana na ubaguzi wa rangi.

Kwa mujibu wa tawimu za Shirika la Utafiti la Pew ambazo zilichapishwa mwka 2017, karibu asilimi 2 ya Wamareiani weusi ni Waislamu, wakiwemo wale ambao wanatokana na vizazi vya watumwa Waislamu Waafrika na pia wale ambao wamesilimu.

3471598

captcha