IQNA

Misikiti yafunguliwa Jakarta Indonesia baada ya miezi mitatu

19:18 - June 05, 2020
Habari ID: 3472838
TEHRAN (IQNA) –Misikiti katika mji mkuu wa Indonesia, Jakarta, imefunguliwa Ijumaa kwa mara ya kwanza baada ya takribani miezi mitatu, huku nchi hiyo ikianza zuio ambalo limekuwepo ili kupunguza kasi ya kuenea ugonjwa wa COVID-19 au corona.

Mbali na misikiti, makanisa na maeneo mengine ya ibada pia yameruhusiwa kuanza shughuli zao katika mji wa Jakarta. Sehemu zingine kama vile maduka, migahawa na maduka zitafunguliwa katika wiki zijazo.

Misikiti imebakia wazi katika maeneo mengine ya Indonesia, nchi yenye idadi kubwa zaidi ya Waislamu duniani.

Hatahivyo, katika mji wa Jakarta, wenye idadi ya watu milioni 30, hii ni mara ya kwanza baada ya miezi mitatu kufunguliwa misikiti.

Walioshiriki katika Swala ya Ijumaa mjini humo wamebainisha furaha yao ya kuweza kushiriki tena katika swala hiyo muhimu katika Uislamu.

Kwa mujibu wa kanuni za afya zilizowekwa, waumini walitakiwa kuleta mazulia au mikeka binafsi ya kuswalia na pia kutokaribiana wakati wa swala huku wote wakipimwa kiwango cha joto mwilini kabla ya kuingia msikitini. Aidha mara hii Swala ya Ijumaa ilikuwa fupi zaidi ya ilivyo ada.

Indonesia ina kesi 29,000 za COVID-19 na hadi sasa watu 1,770 wamefariki kutokana na ugonjwa huo.

Pamoja na hayo, kwa kuzingatia kuwa idadi ya watu nchini humo ni million 260, kiwango cha maambukizi nchini humo kiko chini ikilinganishwa na maeneo mengine duniani.

Hatahivyo watafiti wanaonya kuwa kiwango cha maambukizi na waliofariki ni mara kadhaa zaidi ya idadi rasmi inayotangazwa.

3471599

captcha