IQNA

Misikiti yafunguliwa Nigeria kwa masharti maalumu

19:46 - June 05, 2020
Habari ID: 3472839
TEHRAN (IQNA) –Serikali ya Nigeria imeruhusu misikiti na maeneo mengine ya ibada kufunguliwa nchini humo lakini kwa masharti maalumu huku zuio la COVID-19 likianza kupunguza.

Rais Muhammadu Buhari ameshiriki katika swala ya kwanza ya Ijumaa katika Msikiti wa Ikulu mjini Abuja huku sheria mpya za maeneo ya ibada zikizingatiwa.

Katibu  wa Kamati wa Kifiderali ya Serikali ya Nigeria Boss Mustapa alitangaza mapema wiki hii kuwa kuwa maeneo ya Ibada yataruhusiwa kufunguliwa kwa muda wa saa moja kila wakati na baada ya hapo kufungwa  na kusafishwa kwa dawa za kuua virusi kabla ya kufunguliwa tena.

Kamati ya Kukabiliana na COVID-19 Katika Ofisi ya Rais wa Nigeria imesema maeneo hayo ya Ibada yamefunguliwa kwa muda wa wiki nne kuanzia Juni. Mwenyekiti wa kamati hiyo Sani Aliyu amesema saa za kufunguliwa makanisa na misikiti ni kuanzia saa 11 asubuhu hadi saa mbili usiku kila siku.

Aidha wanaoshiriki katika swala hawaruhusiwi kupeana mikono, kukumbatiana na kukabidhiana chochote. Aidha waumini wanatakiwa kufika msikitini wakiwa wamebeba misala au mazulia ya kuswalia.

Serikali ya Nigeria imesema Madrassah na shule za jumapili zitaendelea kufungwa.   

Hadi sasa watu 11,516 wameambukizwa COVID-19 nchini Nigeria na wengine 323 wamepoteza maisha.

/3902850

captcha