IQNA

Waislamu India hawataweza Kuhiji mwaka huu kutokana na COVID-19

13:00 - June 06, 2020
Habari ID: 3472842
TEHRAN (IQNA) – Kamati ya Hija ya India imesema Waislamu nchini humo hawataweza kusafiri hadi mji wa Makka, Saudi Arabia kutekeleza ibada ya Hija kutokana na janga la COVID-19 au corona.

"Hatujapokea mawasiliano kutoka Saudi Arabia kuhusu Ibada ya Hija mwaka huu.  Aidha itakuwa haiwezekani kwa waumini kutekeleza Ibada ya Hija mjini Makka kutokana na janga la COVID-1," imesema taarifa ya Kamati ya Hija ya India.

Aidha Kamati ya Hija ya India imesema itawarejeshea fedha zao wot ambao walikuwa wameshatoa malipo ya mapema kwa ajili ya kugharamia safari ya Hija.

Kwa sasa safari zote za kimataifa za kutoka na kuingia Saudia kwa ndege zimefutwa kutokana na janga la COVID-19 kama ambavyo India nayo pia imepiga amrufuku safari zote za ndege za kimataifa na hata za ndani ya nchi. Ibada ya Hija mwaka huu inatazamiwa kuanza Julai 30, 2020 kwa kutegemea mwandamo wa Mwezi.

Mwezi Machi Waziri wa Hija wa Saudi Arabia aliwataka Waislamu kote duniani kusitiha kwa muda maandalizi ya ibada ya mwaka huu ya Hija hadi pale hali ya mambo kuhusiana na maambukizi ya virusi vya corona duniani itakapobainika vyema.

Waziri wa Hija wa Saudi Arabia ,Mohammed Saleh Benten amesema, katika mahojiano na televisheni amesema, kwa kuzingatia hali ya sasa ya janga la ugonjwa wa COVID-19 au corona na kwa kutilia maanani kuwa suala la afya ya mahujaji linapewa umuhimu; Saudia inawaomba Waislamu katika nchi zote kusubiri kabla ya kufanya maandalizi ya Hija hadi pale hali itakapoboreka.

Tayari Saudia imeshafuta safari zote za Umrah kwa karibu muda wa miezi miwili iliyopita kutokana na janga la COVID-19.

3471605

captcha