IQNA

Misikiti yafunguliwa tena katika mji mkuu wa Maldivi

18:03 - June 30, 2020
Habari ID: 3472913
TEHRAN (IQNA) – Rais Ibrahim Mohamad Solih wa Malidivi misikiti itafunguliwa tena kuanzia Julai Mosi kwa ajili ya Swala za jamaa katika mji mkuu wa nchi hiyo, Male.

Ni zaidi ya miezi mitatu sasa tokea misikiti ifungwe mjini Male ikiwa ni kati ya hatua zilizochukuliwa kuzuia kuenea ugonjwa wa COVID-19 nchini humo.

Katika ujumbe kupitia Twitter, Rais Solih amesema nchi hiyo imepiga hatua katika vita dhidi ya COVID-19 na sasa umefika wakati wa kuingia awamu mpya ya kufungua maeneo yaliyokuwa yamefungwa. Aidha amesema kuanzia Julai Mosi idara za serikali pia zitafunguliwa huku akiwashukuru wafanyakazi wa sekta ya afya kwa jitihada zao za kukabiliana na COVID-19. Baadhi ya shule zitafunguliwa pia kuanzia kesho katika visiwa  vya nchi hiyo ambavyo havijaathiriwa na COVID-19 huku katika mji mkuu masomo yakianza kwa ajili ya darasa la 9 kwenda juu. Aidha wananchi wametakiwa kuzingatia sheria mpya za kiafya ikiwa ni pamoja na kuvaa barakoa, kutokaribiana na kunawa mikono mara kwa mara.

Hadi sasa walioambukizwa COVID-19 nchini Maldivi ni 2,337 na waliofariki ni 8.

Maldives au Maldivi ni nchi huru kwenye funguvisiwa la Maldivi katika Bahari Hindi katika eneo la kusini mwa Asia. Nchi hiyo inajumuisha  visiwa 1,192 na kati ya hivyo takriban 200 hukaliwa na watu. Idadi ya watu katika nchi hiyo ndogo inakadiriwa kuwa nusu milioni na asilimia 100 ya raia wa nchi hiyo ni Waislamu.

3471843

captcha