IQNA

Mahakama ya Kilele Uturuki

Jumba la makumbusho la Hagia Sophia mjini Istanbul kurejea kuwa Msikiti

12:25 - July 11, 2020
Habari ID: 3472949
TEHRAN (IQNA) - Mahakama ya juu zaidi nchini Uturuki imefungua njia ya jumba la zamani la Hagia Sophia kugeuzwa kuwa msikiti na kubadilisha hadhi yake ya sasa kama jumba la makumbusho.

Baraza la kitaifa la Uturuki lilikubali ombi la mashirika kadhaa yakiliomba kufuta uamuzi wa serikali wa tangu mwaka 1934 unaolipa jumba la Hagia Sophia huko Istanbul hadhi ya jumba la makumbusho.

"Mahakama imeamua kufutilia mbali uamuzi wa baraza la mawaziri ambao uliligeuza jumba hilo takatifu kuwa jumba la makumbusho," imeeleza sehemu moja ya taarifa ya mahakkama hiyo.

Mahakama imebaini kwamba katika vitengo vya mali iliyoandikwa kwa jina la Mehmet Fatih Foundation, iliyopewa jina la mfalme wa utawala wa Othmania  jumba la Hagia Sophia liliorodheshwa kama msikiti na kwamba sifa hii haiwezi kubadilishwa.

Nchi kadhaa, hasa Russia na Ugiriki, ziliionya Ankara dhidi ya kugeuza jumba la makumbusho la Hagia Sophia kuwa mahali pa ibada kwa Waislamu, hatua ambayo Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amekuwa akitakiwa aifanye kwa miaka mingi.

Jumba la Hagia Sophia ni miongoni mwa maeneo yaliyowekwa kwenye orodha ya turathi za duni na Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa, UNESCO, na ni mojawapo ya vivutio vikuu vya watalii huko Istanbul.

Wananchi wa Uturuki na asasi za Kiislamu nchini humo zimeonyeshwa kufurahishwa na uamuzi huo wa mahakama.

Jengo hilo Hagia Sophia lilijengwa mwaka 537 Miladia (CE) na lilipata umaarufu kutokana na kuba lake adhimu na wakati huo lilikuwa jengo kubwa zaidi duniani. Tokea mwaka 537 hadi 1453 lilikuwa ni Kanisa la Mashariki la Kiothodoxi na makao makuu ya Kasisi Mkuu wa Constantinople. Kwa muda mfupi, kati yaani kati ya mwaka 1204 hadi 1261, jengo hilo liligeuzwa na Wapiganaji wa Nne wa Msalaba kuwa Kanisa Katoliki. Wakati watawala wa silsila ya  Wauthmaniya (Ottomans) walipouteka mji huo, mnamo mwaka 1453 Fatih Sultan Mehmet aliagiza jengo la Hagia Sophia litumike kama msikiti. Hadhi hiyo ya Hagia Sophia kama msikiti iliendelea kwa muda wa miaka 482 hadi mwaka 1935 wakati muasisi wa Jamhuri ya Uturuki, Mustafa Kemal Ataturk alipoagiza ligeuzwe na kuwa jengo la makumbusho.

3909715

captcha