IQNA

Qarii wa Misri: Watoto wafunzwe kuhifadhi Qurani wakiwa bado ni wadogo + Video

TEHRAN (IQNA) – Qarii wa Qur'ani kutoka Misri, Sheikh Hani al-Hussaini ametoa wito kwa wazazi Waislamu kuwafunza watoto wao kuhifadhi Qur'ani Tukufu na Tajwid wakiwa bado ni wadogo.

Al-Hussaini amesema ni rahisi zaidi kuwafunza watoto Qur'ani wakiwa bado ni wadogo na kwa hivyo wazazi wanapaswa kuwafunza watoto wao kusoma Qur'ani.

Ameongeza kuwa, kusoma na kuhifadhi Qur'ani Tukufu huwasaidia watoto kuimarisha Imani yao kwa Allah SWT na kujistawisha kimaanawi ni kiakhlaqi.

Al- Hussaini binafsia alifanikiwa kuhifadhi Qur'ani Tukufu kikamilifu akiwa na umri wa miaka 10. Aidha alijifunza misingi ya Tajwidi kutoka kwa Ustadhi mashuhuri Abdullah al-Jawhari.

Al Hussaini alikuwa mwakilishi wa Misri katika Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani ya Malaysia mwaka 2010 ambapo alishika nafasi ya kwanza.

3910632