IQNA

Qiraa ya qarii wa Iran nchini Uturuki + Video

20:04 - July 15, 2020
Habari ID: 3472966
TEHRAN (IQNA) – Klipu fupi ya video ya qiraa ya qarii mkongowe wa Qur'ani Tukufu kutoka Iran imesambazwa katika mitandao ya kijamii.

Klipu hiyo ya mwaka 2007 inamuonyesha Qarii Abbas Salimi wa Iran akisoma sehemu ya aya ya 193 ya Sura Aal Imran isemayo:

رَبَّنَا إِنَّنَا سَمِعْنَا مُنَادِیًا یُنَادِی لِلإیمَانِ أَنْ آمِنُوا بِرَبِّکُمْ فَآمَنَّا؛

"Mola wetu Mlezi! Hakika sisi tumemsikia mwenye kuita akiitia Imani kwamba: Muaminini Mola wenu Mlezi; nasi tukaamini…"

Abbas Salimi alizaliwa mwaka 1953 mjini Tehran na ni mtaalamu wa masuala ya sheria.  Yeye ni miongoni mwa wanchama wa bodi  za usimamizi za Shirika la Darul Qur'an Karim na Taasisi ya Qur'ani ya Ahasanul Hadhith hapa nchini Iran.

Salimu alishika nafasi ya kwanza katika qiraa ya Qur'ani Tukufu katika Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani ya Malaysia mwaka 1979 na ni mwanaharakati wa Qur'ani Tukufu kwa muda mrefu.  Aidha alikuwa Muirani wa kwanza kuwa jaji katika Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani ya nchini Malaysia.

3910506

captcha