IQNA

Mufti Mkuu wa Ghana: Injuzu kuswali Idul Adha nyumbani

19:19 - July 25, 2020
Habari ID: 3472998
TEHRAN (IQNA) – Mufti Mkuu wa Ghana amesema inajuzu kwa Waislamu nchini humo kuswali Swala ya Idul Adha nyumbani.

Kwa mujibu wa tovuti ya myjoyonline.com, Sheikh Osman Nuhu Sharubutu, Mufti Mkuu wa Ghana amesema Waislamu wanaweza kuswali Idul Adha nyumbani ili kuzuia kuenea ugonjwa hatari wa COVID-19.

Taaarifa ya Mufti Mkuu iliyosambazwa na msemaji wake, Sheikh Armiyawo Shaibu, uamuzi wa kuwaruhusu Waislamu kuswali swala ya Idul Adha majumbani umechukuliwa baada ya ushauriano na jamii mbali mbali za Waislamu nchini humo. Amesema uamuzi huo umechukuliwa ili kuzuia kuenea COVID-19.

Halikadhalika Mufti Mkuu wa Ghana amewataka Waislamu wa nchi hiyo kuendelea kuzingatia sheria na kanuni za kiafya kuhusu kuzuia kuenea COVID-19 hasa wakati wa sherehe ya Idul Adha. Aidha amesema watakaotekeleza sunna ya kuchinja wanapaswa kuzingatia kanuni za kiafya. Inatazamiwa kuwa Waislamu watasherehekea Siku Kuu ya Idul Adha Ijumaa 31 Julai mwakaa huu sawa na 10 Dhul Hija 1414 Hijria Qamaria.

3912303/

captcha