IQNA

Wanafunzi kutoka nchi 16 washiriki darsa za Qur’ani za Haram ya Imam Hussein AS

17:59 - August 08, 2020
Habari ID: 3473047
TEHRAN (IQNA) – Kituo cha Qur’ani (Darul Qur’an) katika Idara ya Mfawidhi wa Haram ya Imam Hussein AS huko Karbala, Iraq imeandaa darsa za Qur’ani katika msimu wa joto.

Kwa mujibu wa taarifa ya kituo hicho, wanafunzi kutoka Iraq na nchi 16 wameshiriki katika mashindano hayo kwa njia ya intaneti.

Washiriki wa mashindano ni kutoka nchi kama vile Bahrain, Kuwait, Iran, Oman, Saudi Arabia, Sweden, Denmark, Ujerumani, Australia, Nigeria, Yemen, Pakistan, Marekani Syria, amesema Al Hafiz Muntadhar Al Mansouri, mkuu wa kamati ya mashindano ya Qur’ani katika Idara ya Mfawidhi wa Haram ya Imam Hussein AS.

Amesema jumla ya wavulana na wasichana 1,560 wameshiriki katika darsa hizo na kwamba walikuwa na umri wa baina ya miaka 9 hadi 15.

Masomo hayo ya Qur’ani yamefanyika kwa njia ya intaneti kutokana na vizingiti vilivyowekwa kufuatia kuenea ugonjwa wa COVID-19.

3915084

 

captcha