IQNA

Nasrallah: Vita vya Siku 33 vilithibitisha udhaifu wa utawala wa Kizayuni wa Israel

15:45 - August 15, 2020
Habari ID: 3473068
TEHRAN (IQNA) - Katibu Mkuu wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon amesema Vita Vya Siku 33 vilibadili kanuni za mapigano kwa maslahi ya Lebanon na kuthibitisha utambulisho halisi wa utawala wa Kizayuni na kiwango cha udhaifu wake.

Sayyid Hassan Nasrallah, Katibu Mkuu wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon, aliotoa kauli hiyo Ijumaa usiku alizungumza kwa mnasaba wa mwaka wa 14 wa ushindi wa harakati hiyo ya muqawama katika Vita vya Siku 33 vya Mwaka 2006.

Miaka 14 iliyopita, inayosadifiana na tarehe 14 Agosti 2006, yalimalizika mapigano kati ya siku 33 ya harakati ya Hizbullah ya Lebanon na utawala wa Kizayuni wa Israel baada ya kutolewa azimio nambari 1701 la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ambalo lilikubaliwa na pande hizo mbili. Mapigano hayo yalimalizika kwa ushindi wa Hizbullah na utawala wa Kizayuni wa Israel ulilazimika kurudu nyuma baada ya kupata hasara kubwa.

Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon ameshiria pia kushindwa utawala wa Kizayuni katika vita vya siku 33 mwaka 2006 na kueleza kuwa katika vita hivyo Waisraili kwa mara ya kwanza walipitia tajiriba ya hofu na wasiwasi wa hatari ya kusalia katika eneo utawala huo bandia.  

Katibu Mkuu wa Hizbullah amesema kushindwa Israel katika Vita vya Siku 33 kuliifanya Marekani ianze kutumia mbinu zingine za kutoa pigo kwa Hizbullah ili kuzuia harakati hii kuzidi kuimarika.

Mlipuko wa Beirut

Sayyid Nasrallah, amesisitiza pia kuhusu Hizbullah kujibu uchokozi wowote wa utawala wa Kizayuni. Kabla ya mlipuko wa Beirut mnamo 4 Agosti, utawala wa Kizayuni wa Israel ulikuwa umeingiwa na wasi wasi mkubwa kuhusu uwezekano wa Hizbullah kulipiza kisasi kuuawa mpiganaji wake, Ali Kamil Muhsin, ambaye aliuawa shahidi katika hujuma ya Israel nje kidogo ya mji wa Damascus, Syria. 

Sayyid Hassan Nasrallah katika hotuba yake ya Ijumaa usiku kwa mara nyingine amesema Hizbullah italipiza kisasi dhidi ya utawala wa Kizayuni kufuatia kuuawa mpiganaji huyo wa Hizbullah. Aidha Sayyid Nasrallah pia hakutupilia mbali uwezekano kuwa  utawala wa Kizayuni ulihusika katika mlipuko wa hivi karibuni wa Bandari ya Beirut. Katibu Mkuu wa Hizbullah amesema iwapo itabainika kuwa Israel ilihusika katika mlipuko wa Beirut basi Hizbullah haitanyamazia kimya jinai hiyo na Tel Aviv italipa gharama kubwa kutokana na jinai hiyo.

Mapatano ya UAE na Israel

Nukta ya nne muhimu katika hotuba ya Sayyid Hassan Nasrallah ni kuhusu mapatano baina ya Umoja wa Falme za Kiarabu na Utawala wa Kizayuni wa Israel. Siku ya Alhamisi 13 Agosti, wakuu wa Tel Aviv na Abu Dhabi walitangaza mapatano ya kuanzisha uhusiano rasmi wa kidiplomasia baina ya pande mbili.

Katibu Mkuu wa Hizbullah amesema Umoja wa Falme za Kiarabu na tawala zingine za Kiarabu ni watumwa wa Marekani katika eneo na hivyo mapatano hayo ya Tel Aviv na Abu Dhabi si ya kushangaza. Aidha amesema  kuanzishwa uhusiano rasmi kati ya Umoja wa Falme za Kiarabu na utawala wa Kizayuni ni huduma ya uchaguzi kwa Rais Donald Trump wa Marekani na Benjamin Netanyahu Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni. Aidha amesema hata baada ya mapatano hayo, Marekani ingali inatafakari kuendelea kupora utajiri wa nchi za Kiarabu za Ghuba ya Uajemi.

Hali ya mambo Lebanon

Kuhusiana na hali ya mambo ndani ya Lebanon, Sayyid Nasrallah ameashiria kujiuzulu Hassan Diab kama Waziri Mkuu wa Lebanon na kusema lengo la wanaotaka kuiangusha serikali ya Diab ni kuisukuma Lebanon kuelekea katika vita vya ndani lakini hawatafanikiwa. Sayyid Hassan Nasrallah ameunga mkono wazo la kuundwa serikali ya umoja wa kitaifa Lebanon huku akipinga wazo la kuundwa kile kinachotajwa kuwa 'serikali isiyopendelea upande wowote' na kuongeza kuwa serikali kama hiyo itakuwa ni ya kupoteza wakati.

3472277

captcha