IQNA

Marekani yafedheheka baada ya kushindwa kupitisha azimio dhidi ya Iran katika Baraza la Usalama

16:02 - August 15, 2020
Habari ID: 3473069
TEHRAN (IQNA)- Marekani imefedheheka duniani baada ya kushindwa katika jitihada zake za kulishawishi Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa urefusha muda wa vikwazo vya silaha dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Muswada uliokuwa umependekezwa na Marekani kwa ajili ya kuongeza muda wa vikwazo vya silaha dhidi ya Iran katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa umeshindwa vibaya Ijumaa baada ya kupigiwa kura mbili za kuupinga, mbili za kuukubali huku wanachama 11 wakijizuia kupiga kura.

Azimio ambalo Marekani imelipendekeza katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu kurefushwa zaidi muda wa vikwazo vya silaha dhidi ya Iran halikupata kura zinazohitajika katika baraza hilo siku ya Ijumaa. Azimio hilo la Marekani kwa ajili ya kuongeza muda wa vikwazo vya silaha dhidi ya Iran katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeshindwa vibaya baada ya kupigiwa kura  mbili tu za kuunga mkono kutoka kwa Marekani yenywe na Jamhuri ya Dominican huku wanachama 11 wakijizuia kupiga kura na wengine wawili yaani, China na Russia wakipiga kura ya kulipinga. Hali hiyo imemkasirisha sana Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Mike Pompep. Katika taarifa , Pompeo amesema Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lina jukumu la kulinda na kuhifadhi amani na usalama katika uga wa kimataifa. Ameendelea na taarifa hiyo kwa kudai kuwa,  "Leo baraza hilo limefeli katika jukumu lake la kimsingi kwa kukataa kurefusha vikwazo vya miaka 13 vya silaha dhidi ya Iran."

Hasira za Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani baada ya kupokea jibu hasi kutoka kwa Baraza la Usalama kwa matakwa yaliyo kinyume cha sheria ya Washington kwa mara nyigine ni ishara ya kutengwa Marekani katika uga wa kimataifa hata miongoni mwa waitifaki wake barani Ulaya yaani Uingereza, Ufaransa na Ujerumani.

Mwakilishi wa ujumbe wa Ufaransa katika Baraza la Usalama amesema: "Ufaransa imejizuia kunga mkono azimio ambalo limependekezwa na Marekani kwa sababu yaliyomo katika azimio hilo hayakuwa na jibu sahihi kuhusu changamoto zitokanazo na kufika ukingoni vikwazo hivyo. Aidha kwa sababu kadhaa, azimio hilo halingeweza kuungwa mkono na wanachama wa Baraza la Usalama na halikuwa na misingi ambayo ingeweza kuunganisha mitazamo. Halikadhalika azimio hilo halingeweza kusaidia katika kudumisha usalama na uthabiti katika eneo."

Mwakilishi wa ujumbe wa Ufaransa katika Baraza la Usalama amesema: "Ufaransa imejizuia kunga mkono azimio ambalo limependekezwa na Marekani kwa sababu yaliyomo katika azimio hilo hayakuwa na jibu sahihi kuhusu changamoto zitokanazo na kufika ukingoni vikwazo hivyo. Aidha kwa sababu kadhaa, azimio hilo halingeweza kuungwa mkono na wanachama wa Baraza la Usalama na halikuwa na misingi ambayo ingeweza kuunganisha mitazamo. Halikadhalika azimio hilo halingeweza kusaidia katika kudumisha usalama na uthabiti katika eneo."

Naye Balozi wa Russia katika taasisi za kimataifa mjini Vienna, Austria Mikhail Ulyanov amesema hakuna wasi wasi wowote iwapo Iran itaondolewa vikwazo vya sialaha. Amesema jitihada za Maerkani za kutaka krefusha vikwazo dhidi ya Iran zimefeli kama ilivyotarajiwa.

Ili kufidia kushindwa kwa fedheha siku ya Ijumaa Marekani inakusudia kuanzisha mchakato wa kutatua hitilafu ndani ya JCPOA unaofahamika kwa jina la 'Trigger Mechanism'. Kwa mujibu wa mchakato huu, faili la nyuklia la Iran litarejeshwa katika Umoja wa Mataifa lengo likiwa ni kuanza kutekelezwa tena vikwazo vyote vya Umoja wa Mataifa dhidi ya Iran.

Iran pia imetahadharisha kuhusu kutumika mchakato huo kurejesha vikwazo vya kimataifa dhidi yake. Majid Takhte Ravanchi, mwakilishi wa Iran katika Umoja wa Mataifa ametahadharisha kuwa: "Baraza la Usalama  likilazimisha vikwazo vyovyote au vizingiti dhidi ya Iran basi Iran itatoa jibu kali na haitajiwekea vizingiti katika machaguo yake na Marekani ikichangia katika kuweka vizingiti hivyo au ichukue hatua zozote zilizo kinyume cha sheria,  basi itabeba dhima ya chochote kitakachotokea."

3916623

captcha