IQNA

Jiwe la Ukumbusho la Waislamu waliouawa msikitini New Zealand lazinduliwa

12:00 - September 24, 2020
Habari ID: 3473200
TEHRAN (IQNA)- Waziri Mkuu wa New Zealand amezindua jiwe la ukumbusho katika Msikiti wa Al Noor mjini Christchurch kuwakumbuka Waislamu waliouawa katika hujuma ya kigaidi msikitini hapo mwaka jana.

Jiwe hilo jeusi lenye maandishi ya dhahabu lina maneno yaliyoandikwa “Hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu, na kwake Yeye hakika tutarejea.”

Baada ya kuzinduliwa jiwe hilo, mmoja kati ya wanaoswali msikitini wake alirusha maua hewani na kusema ‘tulipokea risasi na tunarusha maua.”

Waziri Mkuu wa New Zealand aliamkuana na familia za waathirika na kufanya mazungumzo ya faragha nao ndani ya msikiti. Amesema ingawa machungu yamepungua lakini hakuna chochote kinachweza kuondoa uchungu wa kilichojiri msikitni hapo.

Imamu wa Msiktii wa Al Noor, Sheikh Gamal Fouda, amesema jiwe hilo la msingi ni kumbukumbu ya siku ya mauaji na namna nchi hiyo ilivyokabiliana na tukio hilo.

Hayo yamejiri mwezi moja baada ya Mahakama nchini New Zealand kummhukumu kifungo cha maisha jela gaidi Brenton Tarrant baada ya kupatikana na hatia ya kuwaua Waislamu 51 wakati wa swala ya Ijumaa mwezi Machi mwaka jana katika mji wa Christchurch.

Hakimu aliyetoa hukumu hiyo alikiri kuwa hiyo si adhabu tosha kwa jinai ya iliyotendwa na gaidi huyo mwenye itikadi kuwa wazungu ni wanadamu bora zaidi watu wengine wote.

Jaji Cameron Mander wa Mahakama Kuu ya Christchurch amesema Tarrant hajaonyesha kujuta na hiyo hata akibaki jela umri wake wote, adhabu hiyo haiwezi kutosha kufidia jinai zake. Aidha amesema katika hukumu hiyo ya maisha gerezani, Tarrant hatakuwa na haki ya kuomba kupunguziwa adhabu.
"Jinai zako zilikuwa za kishetani sana kiasi kwamba hata ukifungwa hadi ufe gerezani bado hautaweza hautakuwa umeadhibiwa vya kutosha," alisema jaji wakati akitoa hukumu.  Adhabu ya kifo nchini New Zealand ilifutwa katika sheria iliyopitishwa mwaka 2007.

Tarrant, raia wa Australia mwenye umri wa miaka 29, alikiri kutekeleza mauaji ya watu 51 na kujaribu kuwaua wengine 40 na pia amekiri kutekelezx akitendo cha kigaidi katika hujuma ya ufatuaji risasi kiholela dhidi ya misikiti miwili mjini Christchurch.

Gaidi Tarrant pia ni mfuasi sugu wa  Rais Donald Trump wa Marekani ambaye ni mashuhuri kwa chuki dhidi ya Uislamu na Waislamu.

Katika shambulizi la kigaidi la Machi 15 2019 katika misikiti ya Linwood na al-Noor mjini Christchurch, Waislamu 51 waliuawa shahidi na wengine karibu 50 kujeruhiwa.

Jiwe la Ukumbusho la Waislamu waliouawa msikitini New Zealand lazinduliwa

Jiwe la Ukumbusho la Waislamu waliouawa msikitini New Zealand lazinduliwa

Jiwe la Ukumbusho la Waislamu waliouawa msikitini New Zealand lazinduliwa

Jiwe la Ukumbusho la Waislamu waliouawa msikitini New Zealand lazinduliwa

3472620

captcha