IQNA

Jeshi la Yemen limetekeleza shambulizi la ulipizaji kisasi dhidi ya kambi ya kijeshi ya Saudia

13:07 - September 24, 2020
Habari ID: 3473201
TEHRAN (IQNA)- Jeshi la Yemen likishirikiana na vikosi vya kujitolea vya wananchi limetekeleza shambulizi la ulipizaji kisasi dhidi ya kambi ya kijeshi ya Saudi Arabia na kuangamiza askari wasipopungua 10 wa kambi ya adui.

Kanali ya televisheni ya al-Jazeera ya Qatar imeripoti habari hiyo na kuongeza kuwa, shambulizi hilo la kombora la usiku wa kuamkia leo limelenga kambi ya kijeshi ya mamluki wa Saudia katika mkoa wa Saada ulioko karibu na eneo la Dhahran, katika mpaka wa kusini wa Saudia.

Jeshi la Yemen na vikosi vya kujitolea wananchi wa Yemen havijatoa taarifa kuhusiana na shambulizi hilo la kombora, lakini duru za habari zinaarifu kuwa, hujuma hiyo ya ulipizaji kisasi imelenga vikosi tiifu kwa kwa rais mtoro wa Yemen aliyejiuzulu na kukimbilia Riyadh, Abdu Rabbu Mansur Hadi.

Mapema mwezi huu pia, harakati ya Ansarullah ya Yemen ililenga kwa kombora la balestiki na ndege zisizo na rubani (droni) maeneo kadhaa ya kistratajia ndani ya mji mkuu wa Saudi Arabia, Riyadh.

Saudia ilianzisha mashambulizi dhidi ya Yemen mwishoni mwa mwezi Machi 2015 kwa lengo la kuiondoa madarakani Harakati ya Ansarullah na kumrejesha madarakani Abdrabbuh Mansour Hadi, rais wa zamani wa nchi hiyo aliyejiuzulu na kukimbilia Riyadh. Hata hivyo hadi sasa Saudia na washirika wake wameshindwa kufikia malengo yao kutokana na kusimama kidete wananchi wa Yemen. 

Mwezi Juni, Kituo cha Haki za Binadamu cha Ainul Insaniya kilitoa ripoti na kutangaza kuwa tokea muungano wa Saudia uanzishe vita dhidi ya Yemen mnamo Machi 26, 2015 hadi sasa watu 16, 672 wamepoteza maisha moja kwa moja kutokana na vita ambapo miongoni mwao kuna watoto 3,742 na wanawake 2,364.

3472618

captcha