Mehdi Qarasheikhlu amesema mashindano hayo yalikuwa yafanyike katika ukumbi lakini kutokana na kuongezeka maambukizi ya corona katika siku za hivi karibuni, imeamuliwa yafanyika kwa njia ya intaneti.
Amesema mchujo wa mashindano umekamilika katika mikoa 31 kote Iran na fainali za kitaifa zitafanyika mwezi ujao. Mashindano hayo ya kila mwaka huwashirikisha mabingwa kutoka kote Iran ambapo vipaji vipya huweza kubainika.