Al Sabah ambaye atakumbukwa kwa juhudi za kidiplomasia za kupigia debe uhusiano wa karibu na Iraq baada ya vita vya Ghuba ya Uajemi vya mwaka 1990, wakati akiwa waziri wa mambo ya nje, pamoja na kutafuta suluhu katika mizozo mingine ya kikanda, amekufa leo Jumanne akiwa na umri wa miaka 91.
Ukanda wa Asia Magharibi au mashariki ya kati, Sheikh Sabah alisifika kwa juhudi zake za kuweka mbele diplomasia ili kusuluhisha mzozo kati ya Qatar na mataifa mengine ya Kiarabu.
Al Sabah aliingia madarakani mwaka 2006, baada ya bunge kupiga kura ya kumuondoa mamlakani mtangulizi wake Sheikh Saad Al Abdullah Al Sabah, siku tisa tu katika utawala wake. Nafasi yake inatarajiwa kujazwa na kaka yake, mfalme Sheikh Nawaf Al Ahmad Al Sabah mwenye umri wa miaka 83.