IQNA

Sheikh Swabah al-Ahmad Jabir as-Swabah ateuliwa kuwa Amir mpya wa Kuwait

11:30 - September 30, 2020
Habari ID: 3473218
TEHRAN (IQNA)- Sheikh Nawaf al-Ahmad al-Jaber al-Sabah ameteuliwa kuwa amiri mpya wa Kuwait baada ya kuaga dunia Sheikh Swabah al-Ahmad Jabir as-Swabah.

Katika ujumbe kupitia Twitter, Spika wa Bunge la Kuwait, Marzouq al Ghanim amesema Sheikh Nawaf al-Ahmad al-Jaber al-Sabah ambaye kabla ya hapo alikuwa na cheo cha Mrithi wa Kiti cha Amiri ameapishwa  leo Jumatano asubuhi.

Sheikh Swabah al-Ahmad Jabir as-Swabah, Amir wa Kuwait ambaye aliaga dunia hapo jana Jumanne tarehe 29 Septemba, alikuwa mpatanishi wa mwisho mkongwe katika eneo la Asia Magharibi.

Sheikh Swabah al-Ahmad Jabir as-Swabah ametawala Kuwait kwa miaka 14 yaani tangu mwaka 2006 hadi wakati wa kuaga kwake hapo jana Jumanne. Katika kipindi cha uongozi wake, Kuwait imeshuhudia amani na utulivu wa ndani katika nyanja tofauti.

3472681

Kishikizo: kuwait Amir
captcha