IQNA

Mabadilishano ya mateka wa vita yaanza baina ya pande hasimu Yemen

20:50 - October 15, 2020
Habari ID: 3473261
TEHRAN (IQNA) - Operesheni ya kubadilisha mateka wa vita baina ya harakati ya Ansarullah ya Yemen na muungano vamizi wa Saudi Arabia imeanza kutekelezwa leo Alkhamisi kwa kuachiwa huru mamia ya mateka wa pande hizo mbili.

Opresheni hiyo imeanza baada ya harakati ya Ansarullah ya Yemen kuachia huru mateka wawili wa Kimarekani na mabaki ya mwingine mwenzao mkabala wa kuachiwa huru mateka 240 wa harakati hiyo waliokuwa wakishikiliwa na Saudia na washirika wake.

Viongozi wa serikali kibaraka ya waitifaki wa muungano wa Saudia huko kusini mwa Yemen wamesema kuwa, kundi la kwanza la mateka 230 wa Ansarullah na jeshi la taifa la Yemen limewasili katika uwanja wa ndege wa Seyoun katika mkoa wa Hadhramaut na kwamba litasafirishwa kwa ndege ya Shirika la Kimataifa la Msalaba Mwekundu na kupelekwa San'aa. Wameongeza kuwa wakati huo huo ndege nyingine yenye mateka wa kivita wa muungano wa Saudia ilipangwa kuondoka Sana'a ikielekea uwanja wa ndege wa Seyoun.

3929473

captcha