IQNA

Waislamu Uganda sasa wanamiliki kituo cha televisheni

19:00 - October 26, 2020
Habari ID: 3473298
TEHRAN (IQNA) – Baraza Kuu la Waislamu Uganda (UMSC) limefanikiwa kumiliki televisheni kwa ajili ya kueneza mafundisho ya Kiislamu na harakati za Kiislamu.

Katibu Mkuu wa UMSC  Ramadhan Mugalu amesema televisheni hiyo ambayo itajulikana kama Bilal TV, amesema televisheni  hiyo itakuwa daraja la kuwaunganisha waumini na misikiti hasa wakati huu wa janga la corona.

Mapema mwezi Machi mwaka huu, serikali ya Uganda ilifunga maeneo ya ibada ikiwa ni pamoja na misikiti ili kuzuia kuenea corona. Mugali amesema UMSC imejaribu kutumia radio na mitandao ya kijamii kutangaza Uislamu katika kipindi hiki cha corona.

Ameongeza kuwa UMSC imekuwa na mpango wa kuanzisha televisheni ya kitaifa ya Waislamu na kwamba hatua hiyo imeshika kasi baada ya janga la corona. Hivi sasa kuna radhio kadhaa za masafa ya FM ambazo zinamilikiwa na Waislamu kama vile Bilal FM inayomilikiwa na UMSC, Sauti ya Afrika inayomilikiwa na Jumuiya ya Kimataifa ya Wito wa Kiislamu na Pearl FM yenye mmiliki binafsi.

3931303

captcha