IQNA

Familia ya Sheikh Abdul-Basit yaitunuku zawadi Radio ya Qur’ani Misri

22:19 - November 22, 2020
Habari ID: 3473384
TEHRAN (IQNA)- Familia ya qarii maarufu zaidi wa Qur’ani Tukufu wa Misri, Sheikh Abdul-Basit Abdul-Swamad imeitunuku Radio ya Qur’ani ya Misri kanda za qiraa ya qarii huyo.

Kwa mujibu wa taarifa, silsila hiyo ya qiraa imekabidhiwa wakuu wa Radio ya Qur’ani ya Misri katika halfa iliyofanyika Cairo hivi karibuni.

Silsila hiyo ya qiraa ilirekodiwa mwaka 1986 nchini Morocco, miaka miwili kabla ya kuaga dunia qarii huyo, kufuatia ombi la Mfalme wa Pili wa Morocco.

 

هدیه قرآنی خانواده عبدالباسط به رادیو مصر + عکس

Sheikh Abdul Basit Abdul Samad alizaliwa mwaka 1927 katika kijiji cha Almazaizah katika eneo la Armant kusini mwa Misri. Sheikh Abdul Basit Abdul Swamad alikamilisha hifdhi ya Qur'ani akiwa na umri wa miaka 10 kijijini kwake kwa Ustadh Al Amir na akahitimu aina zote za kiraa ya Qur'ani akiwa na umri wa miaka 14.

Abdul Basit alipewa lakabu ya 'Koo ya Dhahabu' kutokana na kiraa yake ya kuvutia na alipendwa mno na wafuatiliaji wa masuala ya Qur'ani kwa kadiri kwamba hadi sasa anatambuliwa kuwa qarii mashuhuri na anayepesndwa zaidi wa Qur'ani.

Qari huyo mashuhuri wa Misri aliaga dunia tarehe 30 Novemba mwaka 1988 katika mji mkuu wa Misri, Cairo.

 

3936505

 

captcha