Hayo yamedokezwa na Bw. Muhsin Muarifi Mkuu wa Idara ya Utafiti wa Ukanda wa Nchi za Kiarabu na Kiafrika katika Chuo Kikuu cha Kimataifa Al Mustafa SAW, ambaye pia aliwahi kuwa mwenyekiti wa Chuo Kikuu cha Kiislamu Ghana, ametaja hayati Rwalings kuwa ni shujaa wa kitaifa Ghana.
Katika mahojiano maalumu na IQNA, ameongeza kwamba Rawlings alikuwa muungaji mkono wa watu waliotengwa na waliodhulimiwa Ghana na pia kote katika bara la Afrika.
Rawlings, aliyeingia madarakani kufuatia mapinduzi mawili ya kijeshi kabla ya kuanzisha utawala wa kidemokrasia nchini mwake, alifariki dunia tarehe 12 mwezi huu wa Novemba akiwa na umri wa miaka 73.
Uhusiano mzuri wa Iran na Ghana
Ameongeza kuwa, uhusiano mzuri ulioko baina ya Jamhuri ya Kiislamu na Ghana hivi sasa ni kati ya turathi zenye thamani za Rawlings. Baadhi ya waandishi wa Ghana katika kumbukumbu zao wameandika kuwa mapinduzi yaliyomleta Rawlings madarakani kwa kiasi fulani yaliiga baadhi ya nadharia za Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran.
Kutetea hakia na uadilifu, kuwasaidia watu waliotengwa na kudhulumiwa katika jamii na kupambana na mabeberu na wakoloni ni nukta za pamoja ambazo zimeyakurubisha mataifa ya Iran na Ghana, amesema Bw. Muarifi.
Misaada ya Iran kwa Ghana
Shahidi Sayyid Hassan Shahcheraghi, ambaye alikuwa mwakilishi wa jimbo la Damghan katika Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge la Iran) katika muongo wa 80 alitembelea Ghana wakati wa urais wa Rawlings na alinukuliwa akisema: “Katika kikao na wakuu wa Ghana, walisema wanafuatilia kwa karibu matukio ya Iran.” Taasisi ya Jihadi ya Ujenzi Mpya ya Iran ilishiriki katika miradi mbali mbali ya maendeleo Ghana wakati wa urais wa Rwalings ikiwa ni pamoja kuwajengia wasiojiweza nyumba na pia kujenga misikiti na shule zaidi ya 200 katika eneo la kaskazini mwa Ghana. Aidha Iran inashiriki katika ustawi wa kilimo nchini Ghana.
Rawlings alitetea Iran
Katika vikao vya kimataifa Rawlings alitetea sana Jamhuri ya Kiislamu ya Iran wakati wa vita vya kulazimishwa vya utawala wa wakati huo wa Iraq dhidi ya Iran.
Bw. Muarifi anasema Rawlings aliwahi kutembelea Chuo Kikuu cha Kiislamu Ghana ambapo aliyapongeza sana Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran.
Wa kwanza upande wa kulia ni Bw. Muhsin Muarifi akiwa na Jerry Rawlings (wa tatu kutoka kulia) katika Chuo Kikuu cha Kiislamu Ghana
Jerry Rawlings, wakati huo akiwa Luteni katika kikosi cha jeshi la wanaanga, alimpindua Jenerali Frederick Akuffo mnamo mwaka 1979 na kuongoza nchi ya Ghana kwa kipindi kifupi na kisha kukabidhi madaraka kwa serikali ya kiraia kabla ya kufanya mapinduzi mengine miaka miwili baadaye, akibaini kwamba serikali ilishindwa kukomesha ufisadi na hakukuwa na uongozi bora.
Kuanzia mwaka 1981 hadi 1993, Jerry Rawlings aliongoza serikali iliyoundwa na wanajeshi na raia. Mnamo 1992, alichaguliwa kuwa rais wa Jamhuri chini ya katiba mpya na alichukua madaraka mwaka uliofuata kwa mihula miwili kabla ya kukabidhi madaraka kwa John Kufour mnamo mwaka 2001.