IQNA

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu

Vikwazo ni jinai ambayo Marekani na washirika wake wa Ulaya wameifanya dhidi ya Iran

22:37 - November 24, 2020
Habari ID: 3473390
TEHRAN (IQNA)- Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesisitiza kuwa: Haiwezekani kuwa na imani kamili na madola ya kigeni na kuwa na matumaini nayo kwa ajili ya kutatua matatizo.

Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, ameyasema hayo leo mjini Tehran katika mkutano na viongozi wa mihimili mikuu mitatu ya dola nchini Iran pamoja na wajumbe wengine wa Baraza Kuu la Uratibu wa Uuchumi. 

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amebainisha kuwa, vikwazo ni ukweli mchungu ambao upo na ni jinai ambayo Marekani na washirika wake wa Ulaya wameifanya dhidi ya taifa la Iran na akaongezea kwa kusema: jinai hii inafanywa kwa miaka kadhaa dhidi ya taifa la Iran lakini imeshtadi katika miaka mitatu ya karibuni.

Ayatullah Khamenei ameashiria njia ya kuvishinda vikwazo na kuvifanya visiwe na athari na akasema: Yumkini njia hii mwanzo wake ikaambatana na tabu na matatizo kadhaa lakini zikifanyika jitihada, ubunifu na kusimama imara kukabiliana na matatizo hayo itawezekana kuvishinda vikwazo; na pale wawekaji watakapoviona havina athari, wataanza taratibu kuviondoa vikwazo hivyo.

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesisitiza pia kuwa, inavyotakiwa, ni kuchukulia kwamba utatuzi hautapatikana kutoka nje ya nchi; na akafafanua kuwa, wale ambao baadhi yetu wanawatumainia, hali za ndani ya nchi zao hazifahamiki hata kidogo zitakuwaje na wala mtu hawezi kuratibu na kupanga mambo yake kwa kutegemea kauli zao.

Ayatullah Khamenei vilevile amegusia maneno ya porojo yaliyotolewa hivi karibuni na nchi tatu za Ulaya na akasema: wao wanaiambia Iran usiingilie masuala ya eneo, wakati wao wenyewe ndio wanaoingilia zaidi na kwa njia isiyo sahihi katika masuala ya eneo; na wakati Uingereza na Ufaransa zina makombora haribifu ya atomiki huku Ujerumani nayo ikiwa inafuata njia hiyo hiyo, zinaiambia Jamhuri ya Kiislamu ya Iran isiwe na makombora.

3473220

captcha