IQNA

Muasisi wa kituo kikubwa zaidi cha Qur’ani Senegal afariki

22:48 - December 27, 2020
Habari ID: 3473499
TEHRAN (IQNA)- Muasisi wa kituo kikubwa zaidi cha Qur’ani Tukufu nchini Senegal amefariki dunia.

Kwa mujibu wa taarifa, Shaykha Maryam Niasse alifariki Jumamosi katika mji mkuu wa Senegal, Dakar.

Shaykha Niasse ambaye alikuwa maarufu kama ‘Mhudumu wa Qur’ani’ alianzisha Kituo cha Elimu ya Qur’ani cha Shaikh al-Islam Hajj Ibrahim Niasse huko Dakar mwaka 1984.

Kituo hicho sasa kimanzisha matawi katika nchi hiyo ya Afrika Magharibi. Shaykha Niase anaenziwa kutokana na jitihada zake za kueneza mafunisho ya Qur’ani na kueneza Uislamu kwa ujumla katika eneo zima la Afrika Magharibi.

Karibu asilimia 93 ya watu wote nchini Senegal ni Waislamu na aghalabu ni Masufi wenye kufuata madhehebu ya Imam Malik.

3943573

captcha