IQNA

Waziri Mkuu wa Canada amteua waziri wa tatu Mwislamu

16:35 - January 13, 2021
Habari ID: 3473554
TEHRAN (IQNA)- Waziri Mkuu wa Canada Justin Trudeau Jumanne amefanya mabadiliko katika baraza lake la mawaziri na kumteua Mwislamu wa tatu katika baraza hilo.

Katika mabadiliko hayo, Trudeau amemteua Omar Alghabra kuwa waziri mpya wa uchukuzi baada ya Navdeep Bains kustaafu.

Alghabra mwenye asili ya Saudia alichaguliwa kama mbunge mwaka 2015  na ana shahidi ya uzamili katika Uhandisi wa Mekaniki  na pia ni mwanaharakati wa kijamii.

Tayari Waislamu wengine wawili wanahudumu katika baraza la mawaziri la Canada ambao ni Ahmad Hussein mwenye asili ya Somalia ambaye ni Waziri wa Familia na Ustawi wa Kijamii na Maryam Monsef mwenye asili ya Afghanistan ambaye ni Waziri wa Maendeleo ya Kimataifa.

3947560

Kishikizo: canada waislamu trudeau
captcha