IQNA

Nusu fainali ya mashindano ya kimataifa ya Qur’ani ya Iran yaanza

21:57 - January 19, 2021
Habari ID: 3473572
TEHRAN (IQNA) – Nusu fainali ya Awamu ya 37 ya Mashindano ya Kimataifa ya Qur’ani Tukufu ya Iran imeanza Jumanne asubuhi mjini Tehran.

Mashindano hayo ya nusu fainali yanafanyika kwa njia ya intaneti kutokana na janga la COVID-19 au corona.

Washiriki wanashindanao katika qiraa au usomaji Qurani Tukufu na pia kuhifadhi Qur’ani Tukufu kikamilifu.

Majaji Wairani katika mashindano hayo wako katika ukumbi wa Shirika la Wakfu la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran huku majaji wa kigeni wakishiriki kwa njia ya intaneti kutoka Syria, Sudan, Iraq, Lebanon na Indonesia.

Mehdi Qarasheikhlu, Mkuu wa Masuala ya Qur'ani katika Shirika la Wakfu na Misaada la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika mahojiano na IQNA, amesema semi fainali ya mashindano hayo inajumuisha washiriki 120 kutoka nchi 70. Washiriki takribani 50 wanatazamiwa kufika fainali ya mashindano hayo ya kusoma na kuhifadhi Qur'ani Tukufu.

Iran Int’l Quran Contest: Semifinal‌ Round Kicks Off

Aidha amesema katika duru za awali kulikuwa na washiriki 600 kutoka nchi 70. Ameongeza kuwa, mashindano hayo ya semi fainali ambayo yanafanyika kwa njia ya intaneti yataendelea hadi Januari 21.

Shirika la Wakfu la Iran huandaa mashindano hayo ya kimataifa ya Qur'ani kila mwaka.

Kutokana na janga la COVID-19 mashindano hayo hayakufanyika mwaka 2020 na yalifanyika mara ya mwish Aprili 2019 mjini Tehran ambapo kulikuwa na washiriki kutoka nchi zaidi ya 80.

3948639  

 

captcha