IQNA

Vituo vya kufunza Qur’ani Qatar vyafunguliwa

19:35 - January 22, 2021
Habari ID: 3473581
TEHRAN (IQNA) – Wizara ya Wakfu na Masuala ya Kiislamu Qatar imetangaza uamuzi wa kufungua tena vituo vya kufunza Qur’ani Tukufu nchini humo.

Taarifa hiyo imesema vituo hivyo vitafunguliwa kwa ushirikiano na Wizara ya Afya ya Umma ili kuzuia kuenea ugonjwa wa corona.

Kwa mujibu wa taarifa vituo  22 vya kuhifadhi Qur’ani Tukufu vya wanawake, vine vya wanaume  na pia vituo vingine 21 jumla vya kuhifadhi Qur’ani vitapata vibali vya kufunguliwa tena.

Vituo hivyo vimefungwa kwa miezi kadhaa kutokana na kuenea corona.

Hadi sasa watu 148 wameambukizwa corona nchini Qatar na miongoni mwao 248 wamefariki.

3473764

Kishikizo: qatar qurani Corona
captcha