IQNA

Misikiti yafungwa Riyadh, Saudia baada ya kuongezeka Corona

21:01 - February 21, 2021
Habari ID: 3473669
TEHRAN (IQNA)- Misikiti saba imefungwa kwa muda katika mji mkuu wa Saudia, Riyadh baada ya waumini saba kuambukizwa Corona au COVID-9.

Kwa kufungwa misikiti hiyo, idadi ya misikiti iliyofungwa kote Saudia katika kipindi cha wiki mbili imefika 105.

Wizara ya Masuala ya Kiislamu Saudia imesema misikiti 92 kati ya hiyo 105 imefunguliwa tena baada ya kusafishwa kwa dawa maalumu za kuua virusi na sasa iko tayari kutumiwa na waumini.

Wizara hiyo imeimarisha ukaguzi wa misikiti ili kuhakikisha inazingatia kanuni za kuzuia maambukizi ya COVID-19 ambayo yameongezeka nchini humo.

Hadi sasa watu 370,000 wameambukizwa COVID-19 nchini Saudia ambapo 6,437 wamepoteza maisha.

3474041/

Kishikizo: saudia misikiti Corona
captcha