IQNA

Taasisi ya Dar Al Ber ya Dubai kuwafadhili waalimu wa Qur’ani duniani

20:35 - February 22, 2021
Habari ID: 3473672
TEHRAN (IQNA)- Mpango mpya umezinduliwa mjini Dubai katika Umoja wa Falme za Kiarabu kwa lengo la kuwafadhili na kuwaunga mkono waalimu wa Qur’ani Tukufu kote duniani.

Mpango huo ambao unajulikana kama ‘Ufadhili wa Waalimu wa Qur’ani’ umezinduliwa na Taasisi ya Dar Al Ber ya Dubai na utajumuisha nchi za mabara ya Asia, Afrika, Ulaya na Amerika.

Mwanachama wa bodi ya wakurugenzi wa Dar Al Ber Khalfan Khalifa Al Mazrui amesema katika kampeni hiyo watakusanya misaada ya kifedha kwa ajili ya waalumu wa Qur’ani katika nchi kama vile Mexico, Indonesia, Ukraine, Sudan, Somalia na Nigeria.

Mpango huo pia unalenga kueneza mafundisho ya Qur’ani yenye kusisitiza umuhimu wa wanaadmau wote kuishi kwa maelewani na kustahamiliana.

3474050

Kishikizo: dubai qurani tukufu ber
captcha