IQNA

Viongozi wa kanisa washiriki katika ufunguzi wa Msikiti Misri

21:06 - February 28, 2021
Habari ID: 3473689
TEHRAN (IQNA)- Viongozi wa kanisa wameshiriki katika ufunguzi wa msikiti katika mji wa El Mahalla nchini Misrikatika jimbo la Gharbia nchini Misri.

Kushiriki viongozi hao wa kanisa katika ufunguzi wa msikiti huo kulikuwa na lengo la kuonyesha ushirikiano na maelewano baina ya Waislamu na Wakristo katika eneo hilo.

Kwa mujibu wa tovuti ya Lomazoma, ujumbe wa kanisa uliongozwa na Adnial Azmi Zaki, kasisi katika kanisa la al Malak Mikhaeil mjini El Mahalla ambaye amesema kufika  msikitini kuna ujumbe wa urafiki baina ya Waislamu na Wakristo mjini humo na Misri kwa ujumla.

Misri ni nchi ya Kiislamu iliyo kaskazini mwa Afrika na idadi ya watu nchini humo inakadiriwa kuwa ni milioni 100. Zaidi ya asilimia 90 ya wakazi wa Misri ni Waislamu na waliosalia ni Wakristo.

3474115

captcha