IQNA

Majaji wa Mashindano ya Kimataifa ya Kimataifa ya Qur’ani ya Iran watangazwa

20:21 - March 03, 2021
Habari ID: 3473698
TEHRAN (IQNA) – Kamati andalizi ya Mashindano ya 37 ya Kimataifa ya Qur’ani Tukufu imetangaza majina ya jopi la majaji katika mashindano hayo.

Kwa mujibu wa taarifa mashindano hayo yatakuwa na majaji 23 kutoka Iran na wengine saba kutoka Sudan, Lebanon, Indonesia, Syria, Tunisia na Jordan. Majaji hao ambao wote ni wataalamu wa Qur’ani watasimamizi zoezi zima la kusoma na kuhifadhi Qur’ani katika mashindano hayo.

Mtaalamu mkongwe wa Qur’ani kutoka Iran, Ustadh Abbas Salimi ataongoza jopo hilo la majaji katika mashindano hayo yatakayofanyika baina ya Machi 6-11.

Mashindano hayo yatafanyika kwa njia ya intaneti na kurushwa hewani mubashara kupitia Televisheni ya Qur'ani ya IRIB, Radio ya Qur'ani ya IRIB na majukwaa mengine ya mtandaoni.

Kauli mbiu ya mashindano ya mwaka huu ni 'Kitabu Kimoja, Ummah Mmoja".

Semi fainali ya mashindano hayo imefanyika mapema mwezi huu kwa njia ya intaneti ambapo kulikuwa na washiriki 120 kutoka nchi 70. Duru za awali za mchujo katika mashindano hayo zilikuwa na washiriki 600 kutoka nchi 70 na zilifanyika pia kwa njia ya intaneti kutokana na janga la corona. Washiriki 57 kutoka nchi 26 watashindano katika fainali za mashindano yam waka huu.

Shirika la Wakfu la Iran huandaa mashindano hayo ya kimataifa ya Qur'ani kila mwaka.

Kutokana na janga la COVID-19 mashindano hayo hayakufanyika mwaka 2020 na yalifanyika mara ya mwisho Aprili 2019 mjini Tehran ambapo washiriki kutoka nchi zaidi ya 80 walishiriki.

3957039

captcha