Kwa mujibu wa Shirika la Iran la Utamaduni na Mahusiano ya Kiislamu (ICRO), mashindano hayo yatafanyika kwa ushiriano baina ya Radio Bilal FM ya Uganda na Kituo cha Utamaduni cha Iran katika nchi hiyo ya Afrika Mashariki.
Hivi karibuni Mwambata wa Utamaduni wa Iran nchini Uganda Mohammad Reza Qezelsofla alifanya mazungumzo na mkurugenzi wa Bilal FM Muzaffar Mungumia kuhusu mashindano hayo ya Qur’ani.
Inatazamiwa kuwa mashindano hayo yatawajumuisha wanafunzi wa shule za Kiislamu za msingi na upili nchini Uganda. Mashindano hayo yatakuwa katikakategoria za kusoma na kuhifadhi Qur’ani Tukufu.
Kwa mara kadhaa sasa Bilal FM imeshirikiana na Kituo cha Utamaduni cha Iran katika kuandaa hafla na mijimuiko ya Kiislamu.