IQNA

Mashindano ya Kimataifa ya Qur’ani yamalizika, Wairani watia fora

20:15 - March 11, 2021
Habari ID: 3473727
TEHRAN (IQNA)- Mashidano ya 37 ya Kimataifa ya Qur’ani ya Iran ambayo yamefanyika kwa njia ya intaneti yalimalizika Jumatano huku washindi wakitunukiwa zawadi.

Sherehe za kuvunga mashindano hayo zimefanyika Tehran na kuhudhuriwa na Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge la Iran) Dkt. Mohammed Baqer Qalibaf, Mkuu wa Shirika la Wakfu la Iran Hujjatul Islam Sayyed Mehdi Khamoushi pamoja na wanaharakati kadhaa wa Qur’ani Tukufu.

Washiriki kutoka Iran walikuwa katika ukumbi na washiriki wengine walijumuika katika sherehe hizo wakiwa katika nchi zao kwa njia ya itaneti kutokana na janga la COVID-19.

Kwa mujibu wa jopo la majaji, Sayyed Hamdi Reza Moqaddasi wa Iran ameshika nafasi ya kwanza katika kategoria ya qiraa ya Qur’ani Tukufu. Kabir Qalandarzadeh wa Afghanistan na Mohammad Ali Qassim wa Lebanon wameshika nafasi ya pili na ya tatu kwa taratibu.

Katika kategoria ya kuhifadhi Qur’ani Tukufu kikamilifu, washindi watatu wa kwanza walikuwa ni Reza Golshahi wa Iran, Mehdi Qorbani wa Afghanistan na Shazad Adin al-Rahman kutoka Marekani.

Washindi katika kategoria ya Tarteel walikuwa ni , Ehsan Mohammadi wa  Iran aliyeshika nafasi ya kwanza Ali Jawad al-Turaihi wa Iraq alikuwa wa pili na wa tatu alikuwa ni Mustafa Sheikh wa Syria.

Katika kitengo cha wanawake kategoria ya kuhifadhi Qur’ani Tukufu kikamilifu, nafari ya kwanza imeshikwa na Atiyeh Tabyanian wa Iran naye Ameneh Sadat Mousavi wa Afghanistan ameshika nafasi ya pili na nafasi ya tatu imechukuliwa na Amani Hassan Seyed Ali kutoka Iraq.

Duru za awali za mchujo katika mashindano hayo zilikuwa na washiriki 600 kutoka nchi 70 na zilifanyika pia kwa njia ya intaneti kutokana na janga la corona. Washiriki 57 kutoka nchi 26 watashindano katika fainali za mashindano ya mwaka huu.

Shirika la Wakfu la Iran huandaa mashindano hayo ya kimataifa ya Qur'ani kila mwaka.

Kutokana na janga la COVID-19 mashindano hayo hayakufanyika mwaka 2020 na yalifanyika mara ya mwisho Aprili 2019 mjini Tehran ambapo washiriki kutoka nchi zaidi ya 80 walishiriki.

3958753

captcha