IQNA

Radio ya Qur’an Qatar yajitayarisha kuukaribisha Mwezi wa Ramadhani

20:48 - April 05, 2021
Habari ID: 3473784
TEHRAN (IQNA) – Radio ya Qur’an ya Qatar imetangaza kuwa tayari kurusha hewani vipindi maalumu vya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Kwa mujibu wa wa taarifa, Abid Muhammad al Shemri, naibu mkurugenzi wa Radio ya Qur’an Qatari, vipindi maalumu vya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani vilianza kutayarishwa miezi minane iliyopita.

Ameongeza kuwa kati ya vipindi watakavyokuwa navyo ni qiraa ya Qur’ani Tukufu ya wasomjai maarufu wa Qur’ani.

Aidha wanazuoni maarufu wanatazamiwa kutoa mawaidha katika idhaa hiyo ya Qur’ani ya Qatar.

3474361

captcha