IQNA

Uingereza yatakiwa itambue rasmi uwepo wa chuki dhidi ya Uislamu

22:26 - April 05, 2021
Habari ID: 3473786
TEHRAN (IQNA)- Serikali ya Uingereza imetakiwa itambue rasmi uwepo wa tatizo la chuki dhidi ya Uislamu yaani Islamophobia ili ikabiliane na tatizo hilo.

Kamati ya Bunge kuhusu Waislamu nchini Uingereza imependekeza kutambuliwa rasmi chuki dhidi ya Uislamu na Waislamu. Katika pendekezo hilo wabunge hao wametaka chuki dhidi ya Uislamu itambuliwe kuwa ‘ni itikadi yenye mizizi ya ubaguzi ambayo inalenga Waislamu au wale wanaodhaniwa ni Waislamu.

Baraza la Uislamu la Uingereza limesema chuki dhidi ya Uislamu imetambuliwa kuwa ni jinai na wabunge na jumuiya za kiraia nchini Uingereza lakini chama tawala cha Wahafidhina au Conservative kimekataa kutambua rasmi uwepo wa tatizo hilo.

Baraza la Uislamu la Uingereza limesema chama cha Conservative kinakana uwepo wa tatizo la chuki  dhidi ya Uislamu miongoni mwa wanachama wake na hivyo hakina hamu ya kutambua uwepo tatizo hilo katika taasisi za Uingereza.

3474367

captcha