IQNA

Janga la virusi vya COVID-19

Waislamu Uholanzi watakiwa kutoalika wageni nyumbani Mwezi wa Ramadhani

18:24 - April 10, 2021
Habari ID: 3473799
TEHRAN (IQNA)-Mwezi Mtukufu wa Ramadhani unatazamiwa kuanza wiki ijayo na Wailsamu takribani milioni moja Uholanzi watajiunga na wenzao duniani katika kufunga Saumu.

Huu utakuwa ni mwezi wa pili wa Ramadhani unaowapata Waislamu katika janga la COVID-19 au corona. Kwa msingi huo Bodi ya Ushirikiano baina ya Waislamu na Serikali ya Uholanzi (CMO), ambayo inawakilisha misikiti 380, imetoa wito kwa familia za Waislamu kubakia nyumbani wakati wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani na kutowaalika jamaa na marafiki ili kuzuia kuenea COVID-19.

“Ramadhani ni wakati wa furaha na kula chakula kizuri lakini huo sio msingi wa mwezi huu mtukufu. Huu pia ni wakati wa kutafakari na kujitathmini,” amesema mwanachama mwandamizi wa CMO Said Bouharrou. Amesema binafsi alikuwa peke yake na familia mwezi mzima wa Ramadhani mwaka jana na kuongeza: “Nilihisi ni wakati wa kipekee na maalumu. Hali hiyo ilinipelekea nijitathmini nafsi na umaanawi wangu.”

Aidha amebainisha wasiwasi wake kuhusu Waislamu kujumuika usiku kwa ajili ya Sala ya Tarawih na Itikafu misikitini wakati huu wa janga la COVID-19. Amesema  katika dini zote kuna hali ya kutoheshimu kanuni za kuzuia kuenea COVID-19 kama ilivyoshuhudiwa katika eneo la Urk ambapo kanisa moja liliamua kupuuzilia mbali kanuni za COVID-19.  Bouharrou amesema waeamua kufunga misikiti yote kuanzia saa nne  usiku. Kwa mujibu wa nyakati za Uholanzi adhana ya Magharibi inatazamiwa kuwa takribani saa moja na dakika 25 mwanzoni mwa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani na kufika saa mbili na dakika 10 mwishoni mwa mwezi huu mtukufu.

3474415

captcha