IQNA

15:22 - April 11, 2021
News ID: 3473802
TEHRAN (IQNA)- Majaji wa Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani ya Televisheni ya Al Kauthar ya Iran wametangazwa.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA,  Awamu ya 14 ya Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani ya Televisheni ya Al Kauthar yatafanyika katika mwezi Mtukufu wa Ramadhani na usajili wa wanaotaka kushiriki ulianza katika siku ya tatu ya mwezi wa Shaaban kwa mnasaba wa kukumbuka kuzaliwa Imam Hussein AS.  

Majaji wa mashindano hayo ni kutoka Iran, Syria, Iraq, Jordan, Misri, Lebanon na Sudan. Majaji hao ni pamoja na Ahmad al Najafi, Rafie al Ameri, Meitham Mumtaz, Natiq Az Zarkani kutoka Iraq, Muutaz Aghai, Mahdi Seif, Sayyid Abbas Anjam, Mohammad Ali Dehdashti na Amir Kismai kutoka Iran. Majaji wengine watakuwa Samii Othmani wa Jordan, Taha Abdul Wahab, Mohammad Kahila na Asfur Mohammad Jabin wa Misri. Aidha wengine watakuwa ni Ridhwan Dariush, Aarif Al Asli na Nurddin Khurshid wa Syria, Adel Khalil na Mustafa Jaafri wa Lebanon na Al Badr Bishara wa Sudan.

Mashindano ya Kimataifa ya Qur’ani Tukufu ambayo huandaliwa na Televisheni ya Al Kauthar yamepewa aya ya Qur’ani Tukufu isemayo  إِنَّ لِلْمُتَّقِينَ مَفَازًا , "Hakika wachamngu wanastahiki kufuzu".  (Qur’ani Tukufu 78:31).

Mashindano hayo, ambayo yametajwa kuwa kati ya makubwa zaidi ya aina yake duniani, hufanyika kwa njia ya simu au intaneti. Kwa maelezo zaidi na kujisajili katika mashindano hayo, tembelea tovuti ya http://mafaza.alkawthartv.com/

Name:
Email:
* Comment:
* captcha: