IQNA

Sheikh Naim Qassim

Kurejea Marekani katika mapatano ya nyuklia ya JCPOA kutakuwa ni ushindi kwa Iran

21:24 - April 12, 2021
Habari ID: 3473804
TEHRAN (IQNA)- Naibu Katibu Mkuu wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon amesema kuwa, kuirejesha Marekani katika makubaliano ya nyuklia ya JCPOA kutakuwa ni ushindi kwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Sheikh Naim Qassim amesisitiza kuwa, wakati Jamhuri ya Kiislamu ya Iran itakapofanikiwa kuirejesha Marekani katika makubaliano ya kimataifa ya nyuklia ya Mpango Kamili wa Pamoja wa Utekelezaji (JCPOA) utakuwa ni ushindi mkubwa kwa Tehran na ushindi wowote wote wa Iran ni ushindi kwa mhimili wa muqawama.

Naibu Katibu Mkuu wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon amezungumzia pia suala la kuundwa serikali mpya nchini Lebanon pamoja na misimamo ya harakati hiyo na kusema kuwa, mhimili wa muqawama ni miongoni mwa makundi ambayo yanafanya juhudi za kuundwa serikali nchini humo na daima umekuwa ukijaribu kukurubisha pamoja mitazanmo mbalimbali. 

Hivi karibuni Sayyid Hassan Nasrullah, Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon alizungumzia mkwamo wa kuundwa serikali nchini humo na kusema kuwa anaamini maadui wa harakati hiyo ya mapambano wanafanya njama za kuanzisha vita vya ndani nchini Lebanon kupitia njia ya kuchochea hitilafu za kisiasa.

Duru ya 18 ya mazungumzo kati ya Saad al-Hariri, Waziri Mkuu wa Lebanon ambaye amepewa jukumu la kubuni serikali mpya, na Rais Michel Aoun, ambayo ilifanyika mwezi uliopita, ilimazika bila natija yoyote ya maana na kwa mujibu wa vyombo vya habari, jambo hilo limeitumbukiza nchi hiyo katika mivutano ya kisiasa ambayo inaweza kuiandama kwa muda mrefu.

3474430

captcha