IQNA

Hizbullah imelaani vikali hujuma ya utawala wa Kizayuni dhidi ya Msikiti wa Al Aqsa

12:28 - April 24, 2021
Habari ID: 3473844
TEHRAN (IQNA) - Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon imetoa taarifa kulaani hatua za kijinai walizofanyiwa hivi karibuni wananchi wa katika mji wa Quds (Jerusalem) unaokaliwa kwa mabavu na kusisitiza mshikamano wake na taifa tukufu la Palestina.

Katika taarifa yake hiyo, Hizbullah imeenzi muqawama wa wananchi wa Palestina na kukabiliana kwao kishujaa na hujuma za Israel dhidi waumini wanaosali katika mji wa Quds unaokaliwa kwa mabavu na ikaongeza kuwa ni jambo la kujivunia kuona jinsi waumini Wapalestina walivyosimama imara katia Bāb al-ʿĀmūd na maeneo mengine mbali mbali ya Quds tukufu inayokaliwa kwa mabavu.

Taarifa hiyo ya Hizbullah imelaani vikali pia hatua za kijeshi na mzingiro ambao polisi wa utawala haramu wa Israel na walowezi wa Kizayuni wamewawekea wananchi wa Palestina tangu siku kadhaa zilizopita hadi sasa na kusababisha makumi ya Wapalestina kujeruhiwa na wengine kadhaa kutiwa nguvuni.

Hizbullah imetilia mkazo pia mshikamano wake kamili na taifa tukufu na la jihadi la Palestina na kuongeza kwamba, taifa la Palestina, ambalo ni dira halisi ya umma wa Kiislamu, limethibitisha kuwa, kujitolea kwake mhanga ni sisitizo kwamba wavamizi maghasibu hawana nafasi katika ardhi iliyotoharika ya Palestina.

Eneo la Bāb al-ʿĀmūd huko Quds inayoakaliwa kwa mabavu, usiku wa kuamkia Ijumaa lilishuhudia mapigano makali baina ya waumini waliokuwa wakisali Wapalestina na askari wa utawala wa Israel pamoja na walowezi wa Kizayuni. Mapigano hayo yalipelekea Wapalestina zaidi ya 100 kujeruhiwa.

3474533

captcha