IQNA

Wabunge wa Majlisi ya Iran wasisitiza kuhusu ulazima wa vikwazo vyote viondolewe

18:48 - May 18, 2021
Habari ID: 3473924
TEHRAN (IQNA) - Wabunge 200 wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge la Iran) wametoa tamko la pamoja la kutaka kufutwa vikwazo vyote ilivyowekewa Iran.

Zaidi ya wabunge 200 wa Iran wamesema katika taarifa yao hiyo ya pamoja kwamba siasa zisizotetereka za Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni kufutwa vikwazo vote  na baada ya Tehran kufanya uchunguzi na kujiridhishwa kuwa ni kweli vikwazo hivyo vimefutwa ndipo nayo itarejea kutekeleza kikamilifu ahadi zake ndani ya mapambano ya nyuklia ya JCPOA.

Katika taarifa yao hiyo wabunge hao wamesema, Bunge la Iran halitambui tofauti wala mgawanyo wowote ambao walioweka vikwazo hivyo wanajaribu kuuaminisha ulimwenguni. Bali Bunge linavihesabu vikwazo vyote kuwa ni sawa sawa, hakuna tofauti yoyote baina yao.

Wabunge wa Iran pia wamesisitiza katika taarifa yao hiyo kwamba, kama vikwazo vyote havitaondolewa kwa asilimia mia moja, basi itakuwa ni kama vile hakuna kikwazo chochote kilichoondolewa.

Tamko hilo limeongeza kuwa, Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge la Iran) itatumia sheria ya hatua ya kiistratijia kwa ajili ya kuhakikisha vikwazo vyote vinafutwa na manufaa ya taifa la Iran yanalindwa, kama ambavyo pia itaendelea kusimamia kwa kina utekelezaji wa mchakato huo.

Wabunge wa Iran vile vile wamesema, tunahimiza na kutilia mkazo kulindwa kikamilifu mafanikio waliyopata wataalamu wa nchi yetu katika sekta ya nyuklia. Tunatilia mkazo jambo hilo katika kalibu ya "Sheria ya Hatua ya Kiistratijia ya Kufuta Vikwazo."

Mazungumzo ya Kamisheni ya Pamoja ya Mapatano ya Nyuklia ya JCPOA katika ngazi ya Manaibu Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na nchi wanachama wa kundi la 4+1, ambalo linajumuisha Russia, China, Ufaransa, Uingereza na Ujerumani pamoja na Umoja wa Ulaya yamekuwa yakifnayika kwa wiki kadhaa sasa Vienna, Austria. 

Mazungumzo hayo ya JCPOA huko yana lengo la kupata njia ya  kuondoa vikwazo vyote vya Marekani dhidi ya Iran, na iwapo vikwazo vitaondolewa na kisha kuwa na dhamana na suala hilo, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran pia itatekeleza tena majukumu yake ndani ya mapatano ya JCPOA. Katika mazungumzo hayo ya Vienna hakuna mpango wowote wa kuondolewa vikwazo hivyo hatua kwa hatua, na suala linalojadiliwa ni kuondolewa mara moja na kwa mpigo vikwazo vyote vya Marekani dhidi ya Iran. 

3972253

Kishikizo: iran jcpoa bunge vikwazo
captcha