IQNA

Jumba la Makumbusho la Bibi Masumah SA mjini Qum, Iran

Jumba la Makumbusho la Haram Takatifu ya Bibi Masumah SAW ni kati ya majumba ya kale zaidi ya makumbusho nchini Iran.

Jumba hilo la makumbusho limehifadhi vifaa vya kale na vyenye thamani kubwa  kutoka karne ya 8 Miladia hadi zama hizi. Kati ya yaliyomo katika jumbo hilo la makumbusho ni Misahafu ya kale. Jumba la Makumbusho la Bibi Masumah SA mjini Qum, Iran lilizinduliwa kwa mara ya kwanza mwaka 1925.