Filamu hiyo inahusu simulizi maalumu ya Ayatullahil- Udhmaa Sayyid Ali Khamenei katika medani za vita vya kulazimishwa vya Iraq dhidi ya Iran hadi katika jaribio la mauwaji la 27/7/1981.
Kwa mujibu wa taarifa ya mwandishi wa IQNA, mwambata wa utamaduni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran mjini Dar es Salaam Murtadha Pirani amepokea nakala ya filamu hiyo hivi karibuni kutoka Salum Bendera ambaye ameitarjumu kwa lugha ya Kiswahili.
Filamu ya matukio ya kweli imeandaliwa katika Taasisi ya Utafiti wa Kiutamaduni ya Mapinduzi ya Kiislamu Ofisi ya kuhifadhi na kueneza athari za Ayatullahil - Udhmaa Sayyid Ali Khamenei
Unaweza kuitazama filamu hiyo katika anuani ifuatayo ya YouTube
https://www.youtube.com/watch?v=aQZHUNItSN4
3979428