IQNA

Haram Takatifu ya Imam Musa al Kadhim nchini Iraq

TEHRAN (IQNA)- Siku kama ya leo miaka 1314 iliyopita alizaliwa Imam Musa al Kadhim ambaye ni mmoja kati ya wajukuu watukufu wa Bwana wetu Muhammad SAW

Alilewa na baba yake Imam Ja'far Swadiq AS na kuchota elimu na maarifa ya Kiislamu kutoka kwa mtukufu huyo kwa kipindi cha miaka 20. Baada ya kuuawa shahidi baba yake, Imam Kadhim AS alishika hatamu za Uimamu na uongozi wa Umma wa Kiislamu kwa kipindi cha miaka 35 na kukabiliana na mashaka mengi. Imam Kadhim AS alipitisha kipindi kingi cha umri wake katika kuwazindua na kuwaelimisha Waislamu maarifa asili ya dini. Suala hili liliwatia hofu kubwa watawala wa Bani Abbas ambao walimkamata na kumfunga jela ili kumuweka mbali na Waislamu waliokuwa na kiu ya maarifa halisi ya dini yao. Imam Kadhim AS alisifika kwa ukarimu mkubwa, uvumilivu na usamehevu. Katika siku hii Haram Takatifu ya Imam Kadhim AS kaskazini mwa Baghdad huwa imepambwa na kuwakaribisha wafanyaziyara kutoka maeneo yote ya dunia.

 
 
Kishikizo: imam kadhim as