Hanine Ashraf Abulaynein ambaye pia alikumbwa na ugonjwa wa saratani akiwa na miaka 9 ni mkazi wa mkoa wa As Sharqiya.
Pamoja na kuwa na changamoto hizo mbili, binti huyo amepata neema ya kuwa mwenye subira na anaendelea kuhifadhi Qur’ani Tukufu na hadi sasa ameshiriki katika mashindano 20 ya Qur’ani Tukufu na kuibuka mshindi.
Mama yake, Bi. Etemad Fathi, 43, anasema bintiye alipata matatizo ya macho akiwa na umri wa miezi 9 na pamoja na hayo alihifadhi Qur’ani Tukufu kikamilifu akiwa na umri wa miaka 7.