IQNA

Hotuba ya Kiongozi Muadhamu katika hafla ya kuidhinishwa rasmi rais mpya wa Iran

17:00 - August 03, 2021
Habari ID: 3474153
TEHRAN (IQNA)- Sherehe za kuidhinishwa rasmi rais wa 8 wa Iran na Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu zimefanyika leo mchana katika Hussainiya ya Imam Khomeini (MA) mjini Tehran ambapo Ayatullah Khamenei, Kiongozi wa Mapinduzi na viongozi wengine wa ngazi za juu wa Mfumo wa Kiislamu wamehudhuria kwa kuzingatia kikamilifu maelekezo na miongozo ya Wazara ya Afya juu ya kujikinga na virusi vya Covid-19.

Katika sherehe hizo Sayyid Ibrahim Raeisi ambaye alishinda uchaguzi mkuu uliopita wa rais ameidhinishwa rasmi na Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kuwa rais mpya wa serikali ya 13 ya Jamhuri ya Kiislamu. Katika hati ya kuidhinishwa serikali hiyo mpya, Kiongozi Muadhamu amesisitiza udharura wa kupewa nafasi tabaka la vijana serikalini, kuondolewa vikwazo vinavyozuia uzalishaji, kuimarishwa thamani ya sarafu ya taifa na kutatuliwa matatizo ya wananchi pamoja na kuwezeshwa katika nyanja tofauti.

Ayatullah Khamanei amesema katika hati hiyo kwamba mahudhurio makubwa ya wananchi katika uchaguzi mkuu uliopita na kuchaguliwa kiongozi huyo ambaye anafahamika kwa sifa zake za kupendwa na watu, unyenyekevu, ucha-Mungu na uzoefu mkubwa na unaong'ara wa uongozi nchini kunathibitisha wazi azma thabiti ya taifa katika kutetea na kufuata njia angavu ya Mapinduzi ya Kiislamu, yaani njia ya uadilifu, ustawi na uhuru.

Huku akiashiria utayari wa nchi kwa ajili ya kufikia maendeleo makubwa zaidi katika nyanja zote, Kiongozi Muadhamu amesisitiza udharura wa kutatuliwa haraka matatizo ya wananchi na kuliwezesha taifa kufikia kiwango na daraja linalostahiki kimaendeleo.

Katika hukumu hiyo ya kumuidhinisha rasmi Ibrahim Raeisi kuwa raia wa serikali ya 13 ya Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran, Ayatullah Khamanei, amemshukuru Mwewnyezi Mungu kwa kuliwezesha taifa shupavu la Iran kushinda mtahani mgumu wa kisiasa na kijamii kupitia uchaguzi na hasa katika kipindi hiki nyeti. Amesema jambo hilo limedhihirisha wazi nafasi muhimu ya wananchi katika uendeshaji na usimamizi wa nchi yao.

Ayatullah Khamenei amesema katika hati ya kumuidhinisha rasmi Sayyid Ibrahim Raeisi kuwa rais wa serikali ya 13 kwamba, leo taifa lina kiu ya kuhudumiwa na kwamba liko tayari kupiga hatua za maendeleo katika nyanja zote kwa kutegemea uongozi bora, wa kijihadi na kishujaa ambao utaliwezesha, na hasa tabaka la vijana kudhihirisha vipawa vyake katika medani ya kazi na uzalishaji nchini.

3988184

captcha